Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Mash Mwana, ameachia rasmi album yake mpya iitwayo “Maajabu the album”.
Album hiyo ina jumla ya mikwaju 12 ya moto huku ikiwa na kolabo 8 kutoka kwa wakali kama Irene Robert, Daddy Owen, Guardian Angel, Levixone,Walter Chilambo,Mr Seed, Jabidii, Didi Man,na Boss MOG.
“Maajabu the album ina nyimbo kama Zungusha, Moto, Never, Nowa,Fanya Njia na tayari inapatikana kwenye mitandao yote ya ku-stream muziki duniani.
Maajabu ni album ya kwanza kwa mtu mzima Mash Mwana tangu aanze safari yake ya muziki mwaka wa 2015.