Staa wa muziki nchini, Otile Brown anaendelea kupokea upendo na support kubwa kutoka kwa mshabiki wake kiasi cha kufanya vizuri na album yake ‘Just In Love’.
Hadi kufikia sasa katika mtandao wa boomplay album hiyo imeweza kusikilizwa zaidi ya mara millioni 17.3 ikiwa ni takriban miaka miwili tangu itokea rasmi.
Kwa mafanakio hayo, Album ya just in love ndio Album iliyosikilizwa zaidi kwenye mtandao wa boomplay kwa wasanii wa humu nchini.
Utakumbuka album ya just in love kutoka kwa mtu mzima otile brown iliachiwa rasmi Juni 3 mwaka wa 2020 ikiwa na jumla ya mikwaju 10 ya moto.