Kundi la muziki wa Hiphop nchini Wakadinali anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Albamu yao ya ” Victims of Madness ” ambayo tayari ina takriban mwaka mmoja tangu itoke rasmi.
Good news ni kwamba Album ya ” victims of madness ” imefanikiwa kufikisha zaidi ya Streams millioni 5 kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay.
Wakadinali ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwashukuru mashabiki zao kwa upendo ambao wanazidi kuwaonyesha kupitia kazi zao za muziki huku likiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi kwa kuachia sehemu ya 2 ya album hiyo.
Ikumbukwe Album ya Victims of madness kutoka kwa kundi la Wakadinali iliachia rasmi machi 4 mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 15 ya moto.