Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba ameachia rasmi albam yake mpya inayokwenda kwa jina la The Only One King.
Album hiyo aliyowashirikisha wasanii tofauti ina jumla ya nyimbo kumi na sita za moto na inapatikana katika platform tofauti na muziki mitandaoni.
Baadhi ya wasanii walioshirikishwa na Alikiba kwenye albam hiyo ni Patoranking kutoka Nigeria, Blaq Diamond, Sauti Sol, Nyashinski, Khaligraph Jones, Sarkodie.
Wengine waliosikika katika albam hiyo ni Mayorkun kutoka nchini Nigeria, Tommy Flavour na K 2ga pamoja na Abdu Kiba kutoka King’s Music.
Ali Kiba ambaye ana miaka zaidi ya 18 kwenye muziki, hii ni album yake ya TATU, ya kwanza ilikuwa ni ‘Cinderella’, iliyotoka mwaka 2006 na ya pili ilikuwa ni ‘Ali K 4Real’,iliyotoka mwaka 2009.
|
|