You are currently viewing ALI KIBA ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA MWAKA WA 2022

ALI KIBA ADOKEZA UJIO WA ALBUM YAKE MPYA MWAKA WA 2022

Hitmaker wa ngoma ya Utu’ msanii Ali Kiba amegusia uwezekano wa kuachia album yake nyingine ifikapo mwakani 2022.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Msanii huyo wa Bongofleva amesema anafikiria kuachia album nyingine mwaka ujao hii ni baada ya album yake mpya Only One King aliyoiachia mwaka huu kufanya vizur kupitia digital platforms mbali mbali.

“Thinking of releasing another album 2022!!!”..ameandika Ali Kiba kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mpaka sasa Ali Kiba ameshaingiza sokoni album tatu na endapo ataachia album mpya mwaka 2022 itakuwa ni album ya nne tangu aanze safari yake ya muziki

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke