You are currently viewing Ali Kiba ampongeza Marioo kwa Album

Ali Kiba ampongeza Marioo kwa Album

Msanii wa Bongofleva, Alikiba amempongeza Marioo kwa kuweza kuachia albamu yake ya kwanza tangu kuanza muziki inayokwenda kwa jina la ‘The Kid You Know’.

Albamu hiyo yenye nyimbo 17, ilitoka rasmi Desemba 9, huku Alikiba akiwa ni miongoni mwa wasanii walioshirikishwa, Kiba kasikika kwenye ngoma, I Miss You.

“Hongera sana mdogo wangu Marioo kwa Albamu yako, The Kid You Know, Inachukua nguvu, akili na utayari kukamilisha albamu hii ni hatua kubwa sana. Nafurahi kuona tumeweza kufanya mziki mzuri” ameandika Alikiba kwenye Twitter.

Kando na Alikiba, wasanii wengine walioshirikishwa ni Rayvanny, Jux, Loui na wengineo, huku ikijuisha nyimbo zake tatu ambazo tayari zimeshatoka Mi Amor, Naogopa na Dear EX.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke