Nyota wa muziki nchini Tanzania, Ali Kiba ameaonesha furaha yake kushirikishwa kwenye album mpya ya Rapa Khaligraph Jones, iitwayo ‘Invisibale Currency’.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Ali Kiba amemshukuru papa jones kwa kumpa shavu kwenye invisible currency album huku akipigia debe album hiyo iliyoachiwa rasmi Machi 07 mwaka wa 2022 ikiwa na jumla ya nyimbo 17 za moto.
Khaligraph jones alimshirikisha ali kiba kupitia wimbo namba 9 uitwao “Wanguvu”. Wasanii wengine walioshirikishwa kwenye album ya mtu mzima khaligraph jones ni pamoja na Prince Indah, Mejja, Balck Way, Adasa, Kev The Topic, Scar Mkadinali, Xenia Manasseh, Rubeboy na Dax.