You are currently viewing ALI KIBA ATANGAZA TOUR YA KUIPROMOTE ALBUM YAKE “ONLY ONE KING”

ALI KIBA ATANGAZA TOUR YA KUIPROMOTE ALBUM YAKE “ONLY ONE KING”

Nyota wa  muziki wa Bongofleva kutoka Kings Music, Ali kiba ametangaza tour kwa ajili ya albamu yake mpya, Only One King.

Albamu ya Only One King ilitoka Oktoba 7, mwaka wa 2021 ikiwa na ngoma 16 za moto alizowashirikisha wasanii kutoka Tanzania, Ghana, Afrika Kusini, Nigeria na Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kings Music, Tour hiyo itaanza Desemba 17, mwaka wa 2021 mkoani Mwanza.

“Mapokezi ya Only one King yamekua makubwa sana!! Asanteni sana fans wa Kings Music na wapenda Mziki mzuri Alalikiba and December is here, let’s get the Party started, I’m officially announcing ONLY ONE KING TOUR IS ON” wameeleza.

Ikumbukwe  hii ni albamu ya tatu kwa mtu mzima Ali kiba, baada ya Cinderella  ya mwaka wa 2007, na Ali K4Real  ya mwaka wa 2009.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke