You are currently viewing ALI KIBA AVUNJA KIMYA CHAKE BAADA YA NDOA YAKE KUFIKA MAHAKAMANI

ALI KIBA AVUNJA KIMYA CHAKE BAADA YA NDOA YAKE KUFIKA MAHAKAMANI

Hitmaker wa ngoma ya “Utu” Msanii Ali Kiba amefunguka kwa mara ya kwanza tangu kuripotiwa kwa taarifa ya mke wake Amina Khalef kufika mahakamani kwa ajili ya kesi ya kuomba talaka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ali Kiba ameandika ujumbe unao ashiria huzuni kufuatia ndoa yake hiyo iliyodumu kwa miaka mitatu kuelekea ukingoni, kwa kumtakia heri mtoto wake Keyaan katika kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa;  “Halizuki jambo bila Mwenyezi Mungu kutaka yote Kheri, Happy birthday Son nakupenda sana, Usinisahau”

Juzi kati taarifa kutoka kwenye magazeti makubwa nchini Kenya zilidai, Mkewe Ali kiba, Amina Khalef amewasilisha kesi katika mahakama ya Kadhi mjini Mombasa kutaka kutengana mume wake.

Alieleza kuwa sababu kuu ya kuvunja ndoa yake na mwanamuziki huyo, ni kuwa na msongo wa mawazo na kutelekezwa na mumewe, huku akidai kuwa Ali kiba hatekelezi majukumu kama mume.

Taarifa zilidai kwa sasa Amina anataka talaka na zaidi ya Shillingi laki 2 kila mwezi kwa ajili matunzo ya watoto. Mahakama imempa Alikiba siku 15 kujibu vinginevyo mchakato wa talaka utaendelea bila yeye kuwepo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke