You are currently viewing Ali Kiba awajia juu mameneja wa WCB kwa kutumia jina lake vibaya

Ali Kiba awajia juu mameneja wa WCB kwa kutumia jina lake vibaya

Staa wa muziki wa Bongo Fleva Ali Kiba ameamua kutoa ya moyoni baada ya Mameneja kutoka lebo ya WCB, Babu Tale na Sallam SK kutoa list ya wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka 2022.

Kwenye orodha hiyo katika List alioiweka Sallam SK amewekwa nafasi ya 7 huku kwenye List ya BabuTale hayupo.

Sasa kupitia ukurasa wake wa Instagram King Kiba amesema wawili hao wanajaribu kutumia jina lake kutengeneza mazingara ya kuitangaza show ya Diamond Platnumz itakayofanyika Desemba 31 mwaka huu.

“I think mmeshajulika kama nilazima mchokenolewe, Ndio mfunction ,ili jambo lenu liende, mmekaa kikao kujadili na kurank wasananii. WHO ARE YOU? Nitaongea jambo lenu likiisha”, Alisema.

Kwenye ujumbe wenye mafumbo ndani yake, ameonekana kumlaumu msanii Harmonize kwa kitendo cha kuzungumzia orodha hiyo kwa kusema imewapa nguvu zaidi kufanikisha jambo lao kwa kuwa wamezoea kutumia kiki kwenye shughuli zao.

“Nilitamani kumwambia Njomba kimbulu asiwachokunoe maana mtakua mmekamilisha malengo yenu kwabahati mbaya Njomba Hajawagundua ila mimi nawajua vizuri for your . Najua hata hiki nilicho kiongea hapa kitawasaidia kwasababu mimi ni KING wenu,” Aliongeza.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke