Hatimaye orodha ya nyimbo ambazo zinaunda Album ya Mfalme wa muziki wa Bongo Fleva ali kiba iitwayo Only One King imeachiwa rasmi.
Album hiyo ina jumla ya nyimbo kumi na sita na kwa sasa unaweza kui-pre order kupitia mtandao wa kusambaza muziki duniani wa Apple Music.
Kwenye Album hiyo wasanii mbalimbali kama patoranking, black diamond, sauti sol, nyashinski, khaligraph jones, sarkodie, Mayorkun, tommy flavour, k2ga na abdu kiba ndio watasikika
Nyimbo 12 kwenye album hiyo ndio geni haujawahi kuzisikia masikioni mwako na nyimbo 4 tu ndizo ambazo Ali kiba ameshaziachia tayari.
Only one king Album kutoka kwa mtu mzima Ali kiba inatoka Oktoba 7, mwaka wa 2021 kwenye mitandao ya kusambaza muziki duniani.