Tuzo za Tanzania Music Awards 2021 zimetolewa usiku wa kuamkia Aprili 3 huko Jijini Dares-Salaam, nchini Tanzania ambapo nyota wawili wa muziki wa BongoFleva, Ali Kiba na Harmonize wameibuka na ushindi kwenye vipengele vingi zaidi.
C.E.O wa Kings Music, Ali kiba ameibuka mshindi na tuzo 5 za Tanzania Music Awards (TMA) kwenye vipengele vya Album bora (One Only King), video bora ya mwaka (Salute FT RudeBoy), mtunzi bora wa mwaka, Mwanamuziki bora wa Afrika Mashariki na Mwanamuziki Bora wa Kiume Chaguo la Watu mwaka 2021.
Kwa upande wa Harmonize, yeye ameshinda tuzo 3 za Tanzania Music Awards kwenye vipengele vya Mtumbuizaji bora wa kiume, Msanii bora wa mwaka na Kolabo bora Afrika (Attitude ya Harmonize FT Awilo Longomba).
Wasanii wengine walioshinda tuzo hizo ni pamoja na Nandy, Professa Jay, Darassa, Marioo, Diamond Platnumz, Young Lunya, Chemical, Saraphina, Baddest 47, Snura, Sholo Mwamba, Khadja Yusuph, Mzee Yusuph na wengine wengi.