Mwanamuziki Alicia Keys kutoka nchini Marekani, hajataka kuumaliza mwaka 2021 bila kuwapa zawadi mashabiki wake. Nyota huyo ametangaza rasmi kuachia album yake mpya iitwayo “Keys”, Desemba 10 mwaka huu.
Amebainisha kuwa album hiyo itakuwa na matoleo mawili (Two versions) yaani itatoka na toleo la Originals na Unlocked.
Upande wa “Original” utakuwa na “Vibes laidback piano,” zinazozalishwa na Alicia, wakati upande wa “Unlocked” utakuwa na “Upbeat, ngoma za vibe ya juu,” zinazozalishwa pia na mrembo huyo kwa kushirikiana na Mike, maarufu Mike Will Made It.
Hii inaenda kuwa album ya Kumi kutoka kwa aliciakeys kwenye muziki wake baada ya alicia ya mwaka wa 2020.