Mahakama ya California imemuhukumu kifungo cha miaka minne mtu mmoja kati ya watatu walioshtakiwa kwa kupora mbwa aina ya Kifaransa wa mwanamuziki maarufu duniani, Lady Gaga.
Jaylin Keyshawn White alikiri kuwa sehemu ya genge lililompiga risasi Ryan Fischer wakati akiwafanyisha mazoezi mbwa watatu mjini Hollywood Februari mwaka 2021.
Katika usikilizaji wa kesi hiyo jijini Los Angeles jana, White, ambaye sasa ana umri wa miaka 20, alikiri kufanya unyang’anyi huo na akapewa kifungo cha miaka mine jela.
Kamera za ulinzi katika eneo hilo la shambulizi zinaonyesha gari ikisimama karibu na Fischer na watu wawili wakirukia nje.