You are currently viewing ALLAN HENDRICK AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA KALIFAH AGANAGA

ALLAN HENDRICK AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA KALIFAH AGANAGA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Allan Hendrick maarufu kama Paper Daddy amepuzilia mbali madai ya kuwa kwenye bifu na msanii mwenzake Kalifah Aganaga.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Allan Hendrick amesema yeye na Kalifah Aganaga ni marafiki wakubwa, hivyo hawana ugomvi wowote kama jinsi ambavyo vyombo vya habari nchini Uganda vimewaaminisha mashabiki wao.

Awali Kalifah Aganaga alimsuta vikali Bebe Cool kwa hatua kumtelekeza kimuziki mwanae Allan Hendrick ambapo alienda mbali zaidi kujitolea kumuandikia nyimbo zitakazo mfanya msanii huyo awe Staa.

Hata hivyo kwenye moja ya mahojiano juzi kati Kalifah Aganaga alinukuliwa akisema kwamba anajutia kumkosoa Bebe Cool na anatamani kumuomba msamaha kwa kumvunjia heshima.

Utakumbuka Allan Hendrick na Kalifah Aganaga tayari wamefanya wimbo wa pamoja ambao wana mpango wa kuachia hivi karibuni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke