Msanii wa Bongofleva Amber Lulu ametunukiwa tuzo ya Silver Play Button na mtandao wa youtube baada ya kufikisha jumla ya subscribers laki moja kwenye chanel yake.
Amber Lulu ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia kazi zake za muziki huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi.
“Asanteni sana my fans asanteni you tube kwa zawadii ni hatua nzur katika safar yangu ya mziki naomba muendelee ku subscribe thanx 🙏,” Ameandika kupitia Instagram
Channel ya youtube ya Amber Lulu ilifunguliwa rasmi Disemba 27 mwaka wa 2016 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 9.7 huku ikiwa na jumla ya subscribers 103, 000.
Itakumbukwa tuzo ya silver play button huwa inatolewa kwa wanamuziki au watu maarufu kwenye mtandao wa youtube ambao hujizolea zaidi ya subcribers laki moja.