You are currently viewing AMBER LULU: NAMTAMANI SANA JUX

AMBER LULU: NAMTAMANI SANA JUX

Msanii wa Bongofleva Amber Lulu amemtaja Juma Jux kuwa ndio mwanaume anayetamani kupata naye mtoto kwa sababu ana akili, yupo smart na atamuongoza vyema lakini pia amekuwa akimfuatilia msanii huyo kwa muda mrefu.

Mrembo huyo ambaye anafanya poa na singo yake mpya iitwayo Nimeachika amesema amepanga kuzaa watoto 5 kila mmoja na baba yake sababu akizaa na baba mmoja kisha akafariki yeye ataishia kupata tabu na watoto.

Ikumbukwe pia Amber Lulu kipindi cha nyuma alishaweka wazi kutamani kuwa kwenye mahusiano na Diamond Platnumz, lakini hata hivyo nafasi ya kuwa na Diamond inaonekana ni nyembamba sababu baada ya hitmaker huyo wa Naanzaje kuzaa watoto 4 na wanawake tofauti amekiri hivi karibuni kuwa kwa sasa kuwa kwenye mahusiano na wanawake sio kipaumbele chake bali nguvu amezielekeza kwenye kuzidi kufanya kazi ili kuendelea kufanikiwa kiuchumi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke