Mwanamintindo na mfanyibiashara, Amber Ray, amezindua lebo ya muziki iitwayo Rich Baddness Record ambapo amemtambulisha msanii wake wa kwanza aitwaye Shifuu ambaye ameachia rasmi video ya ngoma yake iitwayo ‘Monica’
Akizungumza na waandishi wa habari, Amber Ray amesema lengo la kuanzishwa lebo hiyo ni kusaidia vijana wenye vipaji kujitangaza kupitia muziki na pia kuifanya sanaa ya muziki nchini izalishe pato la taifa.
Mrembo huyo ambaye ametamba kwenye mitandao ya kijamii kwa miaka mingi amesema baada ya kumtambulisha msanii wake Shifuu ana mpango pi kutanua wigo wa lebo hiyo kwa kuwaongeza wasanii wengine wenye vipaji nchini.
Hata hivyo ameomba mashabiki wa muziki nchini kumuunga mkono ili aweze kusonga mbele maana kwa sasa amekuwa na watu kadhaa ambao wamekuwa wakimtegemea katika kufanya sanaa ya muziki.
Rich Baddness Record inakuwa ni lebo ya kwanza nchini Kenys kuanzishwa na kusimamiwa na mwanamitindo, ikilinganishwa na lebo kadhaa ambazo zilikuwa zikisimamiwa na wadau waliokuwa katika tasnia ya sanaa na burudani.