You are currently viewing AMBER ROSE AFUNGUKA KUHUSU TWEET YAKE  YA MWAKA 2015 INAYOONEKANA KUMPONZA EX WAKE KANYE WEST

AMBER ROSE AFUNGUKA KUHUSU TWEET YAKE YA MWAKA 2015 INAYOONEKANA KUMPONZA EX WAKE KANYE WEST

Mwanamitindo kutoka Marekani, Amber Rose amevunja kimya chake kuhusu sakata linaloizingira ndoa ya  Kim Kardashian na Kanye West baada ya watu kumkumbusha tweet yake ya zamani aliyomponda Kanye West.

Tweet hiyo aliyoipost mwaka 2015 baada ya kuachana na Kanye West ilisomeka  “Kanye West, nitawaachia ‘Kartrashians’ wakudhalilishe pale ambapo watakuwa wamemalizana na wewe.”

Hiyo ilikuwa baada ya Kanye West kufanya mahojiano na kituo cha break fast club na kusema kuwa ilimbidi aoge mara 30 kabla ya kukutana na familia ya The Kardashians kutokana na uchafu wa aliyekuwa Ex wake Amber Rose.

Baada ya mashabiki kumkumbusha tweet yake hiyo katika hali ya kumbeza Kanye West ambaye amekuwa akipitia wakati mgumu kutoka kwa familia ya Kim, Amber Rose ameibuka na kusema tweet hiyo ilikuwa ni ya zamani na kwa sasa alishajifunza kutokana na makosa yake, hivyo hawezi kuingilia maisha ya familia yeyote na The Kardashians hawakutakiwa kuambiwa maneno kama yale.

Utakumbuka Amber rose na Kanye west walikuwa kwenye mahusiano kati ya  mwaka 2008 na 2010 lakini walikuja wakaachana baada kanye west kuingia kwenye mahusiano na baby mama wake kim kardashian

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke