You are currently viewing Amber Rose mbioni kuandika kitabu kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake

Amber Rose mbioni kuandika kitabu kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake

Mwanamitindo maarufu duniani Amber Rose ameibuka na kudai kuwa kuna unyanyasaji mkubwa sana wa wanawake lakini vyombo vya habari vimekuwa na upendeleo pale mwanamke anapojitokeza kuongea ukweli.

Amber amefunguka kuwa ndio maana huchukua miaka mingi kwa mwanamke kuja kuzungumza unyanyasaji alioupitia kwenye maisha yake kwani wakijitokeza mapema huitwa waongo.

Mwanamama huyo ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kuwa kwenye mahusiano na Rapa Kanye West, ameahidi kuandika kitabu kwani hawezi kufunguka yote kupitia mitandao ya kijamii. Lakini pia amesema atachangia wale wote waliothirika na dhuluma za kijinsia.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke