You are currently viewing ANGELINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

ANGELINA ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Nyota wa muziki nchini uganda Angelina amedokeza mpango wa kuachana kabisa na masuala ya muziki.

Angelina ameweka wazi hayo kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo amesema ataacha muziki mwaka wa 2022 baada ya kuachia project yake ya mwisho ambayo amekuwa akiifanyia kazi kwa muda.

Kulingana na mrembo huyo baada ya kuacha muziki ataelekeza nguvu zake kwingine katika suala zima la kujitafutia riziki.

Hata hivyo tweet yake hiyo haikukaa kwa muda kwenye ukurasa wake twitter kwani alikuja akaifuta baada ya kuchapisha.

Angelina amekuwa kwenye kiwanda cha muziki nchini Uganda kwa muda wa miaka kumi na ametoa hits kali kama Go Down, Ghetto Lovin, Ronaldo na nyingine kibao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke