Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Angelina ni moja kati ya wasanii wa kike wanaofanya vizuri kimataifa..
Mrembo huyo mzaliwa wa London, Uingereza ameachia ngoma kali kama Ghetto Loving, Go Down na nyingine ambazo ziliacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.
Sasa akiwa kwenye mahojiano na Galaxy FM Angelina amedokeza mpango wa kuhamia nchini uganda kwa lengo la kuanza kufanya muziki rasmi.
Angelina amesema amejipata anapenda muziki baada ya babake mzazi kuzima ndoto yake ya kuwa mwanasoka mwongo mmoja uliopita.
Hii ni habari njema kwa mashabiki wa mrembo huyo ambao walikuwa wamevunjika moyo mara baada ya kutangaza kuacha muziki mwaka wa 2022 atakapoachia project yake ambayo alidai kuwa amekuwa akiifanyia kazi kwa muda.
Ikumbukwe kwa sasa Angelina anafanya poa na singo yake iitwayo Mercy aliyomshirikisha mkongwe wa muziki kutoka nchini Jamaica Honorable, singo ambayo inafanya vizuri kwenye chati za muziki nchini Jamaica.