You are currently viewing ANGELIQUE KIDJO ASHINDA TUZO YA GRAMMY KUPITIA KIPENGELE CHA BEST GLOBAL MUSIC ALBUM

ANGELIQUE KIDJO ASHINDA TUZO YA GRAMMY KUPITIA KIPENGELE CHA BEST GLOBAL MUSIC ALBUM

Mwanamuziki kutoka nchini Benin, Angelique Kidjo ameibuka mshindi wa kipengele cha Best Global Music Album kwenye Tuzo za Grammy ambazo zimetolewa usiku wa kuamkia leo.

Kidjo na album yake ‘Mother Nature’ amemuangusha Wizkid kupitia album yake ‘Made In Lagos: Deluxe Edition’ ambayo ilikuwa inapewa kipaumbele.

Lakini pia Wizkid amepata pigo nyingine baada ya mwanamuziki Arooj Aftab  kutoka Pakistan kumshinda kwenye kipengele cha best global music performance kupitia ngoma yake ya mohabbat.

Arooj Aftab amewashinda wikzkid kupitia ngoma yake ya Essence, na Burna boy kupitia wimbo wake wa Do Youself aliyomshirikisha Angelique kidjo pamoja.

Utakumbuka Wizkid alitajwa kuwania tuzo za grammy mwaka wa 2022 kupitia vipengele viwili ambavyo ni Best Global Music Perfomance kupitia ngoma ya Essence na Best Global Music Album kupitia album yake ya Made In Lagos: Deluxe Edition.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke