Msanii wa kike nchini Uganda Angellla Katatumba anaamini kuwa yeye ni moja kati ya wasanii wanaozungumziwa nchini humo licha ya kutoachia magoma makali.
Kupitia mitandao yake ya kijamii ameibuka na kujinasibu kuwa ana neema ya kuzungumziwa kwa kila anachokifanya kwenye maisha yake.
Hata hivyo mashabiki zake wametofautiana kimawazo na mrembo huyo wakimtaka aache kuzungumza vitu ambavyo havina msingi na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye suala la kuachia muziki mzuri.
Angella Katatumba, ambaye ana umri wa miaka 46, amekuwa kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda kwa muda mrefu bila kuachia hitsongs yeyote ila jina lake limekuwa likizungumziwa nchini humo kwa kujihusisha na kashfa mbali