You are currently viewing ANJELLA KUACHIA EP MPYA MWEZI DISEMBA MWAKA 2021

ANJELLA KUACHIA EP MPYA MWEZI DISEMBA MWAKA 2021

Nyota wa kizazi kipya ktoka lebo ya Konde Gang, msanii Anjella ametangaza rasmi ujio wa Extended Playlist (EP) yake mpya na ya kwanza tangu aanze muziki.

Anjella ambaye hupenda kujiita ‘The Black Angel’ ame-share taarifa hiyo kupitia insta story yake na kusema EP itaingia sokoni Disemba 5 mwaka wa 2021 ambapo hajaweka wazi ameipa jina gani.

Akiwa tayari ana miezi nane tangu atambulishwe rasmi Machi 11 mwaka huu na lebo yake ya konde gang kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania, Anjella tayari ana jumla ya ngoma 4, ambazo  ni “Kama”, “Nobody”, “Nobody Remix” na “Sina Bahati”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke