Mwimbaji wa nyimbo za Injili Annastacia Mukabwa, amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Maurice William Juma .
Taarifa hizo zimethibitisha na marafiki zake wa karibu baada ya kuachia picha za baadhi ya matukio ya Harusi yao ambayo ilifanyika katika Kanisa Kuu la Praise huko Imara Daima, Nairobi Desemba 10.
Harusi hiyo ilihudhuriwa na waimbaji kadhaa mashuhuri wa nyimbo za Injili, akiwemo Evelyne Wanjiru, Lady Bee na Solomon Mkubwa.
Hata hivyo mastaa mbali mbali na mashabiki wake wamempongeza kwa hatua hiyo huku wakimtakia mema na mume wake katika safari yao ya ndoa.