You are currently viewing ANNASTACIA AJITAPA WIMBO WAKE NDIO CHANZO CHA RINGTONE KUACHA MUZIKI.

ANNASTACIA AJITAPA WIMBO WAKE NDIO CHANZO CHA RINGTONE KUACHA MUZIKI.

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Annastacia Mukabwa, amefunguka kwa mara ya kwanza baada msanii mwenzake Ringtone Apoko kutangaza kuacha muziki wa injili.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Mukabwa amesema wimbo wake uitwao Kaa Kando ndio umempelekea Ringtone kuchukua maamuzi magumu ya kuacha muziki wa injili kwa sababu amekuwa akitumiwa na shetani kuichafua tasnia ya muziki huo nchini.

“After releasing this Song Kaa Kando naona watu waliokuwa wamejificha ndani ya Gospel industry as Gospel artist wameanza kukaa Kando,” Amesema.

“Wanatumiwa na shetani kuchafua sifa ya injili. Mungu anawaanika mmoja baada ya mwengine,” Ameongeza.

Kauli yake imekuja mara baada ya Ringtone Apoko kudai kuwa wanawake waliokuwa wanamtaka kimapenzi ndio walimfanya akaacha muziki wa injili ambapo alienda mbali zaidi na kuwashauri wamfuate Yesu Kristo.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke