You are currently viewing APPLE WAONDOA UDHAMINI WAO KWA KANYE WEST BAADA YA KUTANGAZA MSIMAMO WAKE KUHUSU ALBUM YA DONDA 2

APPLE WAONDOA UDHAMINI WAO KWA KANYE WEST BAADA YA KUTANGAZA MSIMAMO WAKE KUHUSU ALBUM YA DONDA 2

Kampuni ya Apple imetangaza kuondoa kiasi cha shilling billion 2.3 pamoja na kuondoa udhamini wake kwa Kanye West ambaye mishoni mwa wiki iiliyopita alitangaza rasmi kuwa album yake mpya “DONDA 2” itapatikana kwenye Jukwaa lake la ‘Strem Player’ kifaa maalum cha kusikiliza muziki.

Kupitia ukurasa wake wa instagram wiki iiliyopita, Kanye West alifunguka makubwa ikiwemo kuyakandia maduka maarufu ya kuuza muziki mtandaoni ikiwemo Apple, Amazom, Spotify na YouTube akisema kwamba inawanyonya wasanii ambao hupata asilimia 12 pekee kwenye kazi zao. Hivyo ni muda wa wasanii kuanzisha maduka yao ya kuuza muziki.

Stem Player, ni kifaa maalum ambacho kitauzwa kwa zaidi ya shilling elfu 19. Kwa mujibu wa The Daily Mail, Kanye West tayari ametengeneza kiasi cha shilling million 154 ikiwa ni ndani ya masaa 12 ya tangazo lake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke