You are currently viewing ARNELISA AFUNGUKA WANAUME KUPENDA PESA ZAKE WANAPOKUWA KWENYE MAHUSIANO NAYE

ARNELISA AFUNGUKA WANAUME KUPENDA PESA ZAKE WANAPOKUWA KWENYE MAHUSIANO NAYE

Mrembo na Mjasiriamali nchini, Anerlisa amesema kuna ex wake alitaka amfungulie biashara jambo ambalo alilikataa na huo ukawa mwisho wa kuachana.

Kupitia instastory yake amezungumzia pia suala la kuomba fedha kila wakati katika mahusiano kitu ambacho alikuja kubaini kuwa watu wanaenda kwake kwa ajili kujinufaisha na sio mapenzi.

“Nilikuwa kwenye mahusiano ambapo mwenzi wangu alianza kuniambia nimwambie PIN ya ATM, wakati mwingine nikiongea na mama yangu anataka kujihusisha na mazungumzo yetu” amesema

“Wacha nicheke mmoja wa ex wangu aliniuliza tumekuwa pamoja kwa mwaka mmoja kwa nini nisimsaidie kama vile kumjengea nyumba na hata kumfungulia kampuni kama yangu, nilimjibu ni kamwambia kama uliona kuanzisha uhusiano na mimi kutakutajirisha haya basi uko kwenye uhusiano ambao haufai,” amesema Anerlisa.

Utakumbuka Anerlisa aliwahi kuolewa na Staa wa Bongofleva, Ben Pol lakini ndoa yao ikadumu kwa muda mfupi, katika mapenzi yao mrembo huyo alitokea kwenye video ya wimbo wake Ben Pol, Kidani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke