You are currently viewing Arnelisa yupo uhuru, Akamilisha talaka yake na Mwanamuziki Ben Pol

Arnelisa yupo uhuru, Akamilisha talaka yake na Mwanamuziki Ben Pol

Ni rasmi kuwa mfanyabiashara wa Kenya Anerlisa Muigai na mwanamuziki kutoka Tanzania Ben Pol sio mke na mume tena.

Anerlisa ambaye ni binti wa seneta wa Nakuru Tabitha Karanja kupitia ukurasa wake wa Instagram, amefichua kuwa talaka yake na mwimbaji huyo wa Bongofleva hatimaye imekamilika.

Mrembo huyo amewashukuru mawakili wake kwa kuhakikisha kuwa mchakato wa talaka yake umekamilika

“Niko huru rasmi. Haitakuwa sawa kutowatambua mawakili hawa wawili ambao walifanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kwamba talaka inafanywa haraka na sio kusubiri kwa miaka. Hamza Jabir na Hosea Chamba, asanteni kwa kazi zenu na kwa kufanya kila kitu mlivyoombwa.” alisema kwenye Insta stori.

Anerlisa na Ben Pol walifunga ndoa Mei mwaka 2020 lakini wakatengana mwaka jana ambapo Ben Pol aliwasilisha kesi ya talaka mahakamani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke