Msanii kutoka Uganda Aroma alipata umaarufu kwenye muziki wake kupitia wimbo uitwao Yoola ambao aliwashirikisha wasanii wa B2c Boys.
Tangu wakati huo amekuwa akiachia magoma makali ambayo yanazidi kufanya vizuri kwenye chati mbali mbali za muziki.
Aroma, ambaye amekuwa akifanya na uongozi wa Butterfly Entertainment inaonekana amefanya mabadiliko kwenye kazi yake ya muziki.
Taarifa mpya ni kwamba mrembo huyo amejiunga na lebo ya Team no sleep ambayo inamilikiwa na jeff kiwa na tayari ameachia nyimbo mbili ambazo ni “Omugenyi Omukulu” na “Check Yo Lover”.
Aroma anajiunga na wasanii wengine kama Grenade na Pinky ambao tayari wapo chini ya lebo hiyo.
Aroma alianza muziki mwaka 2018 alipoachia wimbo wake wa kwanza “Wakimala” ambao alirekodi na prodyuza Skales huko Kampala lakini akaachia video yake Julai mwaka wa 2019 ambayo ilimtambulisha kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.