Msanii wa kike kutoka nchini Uganda Aroma amesikitishwa na namna wasanii wakubwa nchini humo wanaendesha tasnia ya muziki.
Akiwa kwenye moja ya interview Aroma amedai kwamba mastaa wengi nchini uganda wamehujumu kazi za wasanii chipukizi kwani wamekuwa na mazoea ya kuzihonga vyombo vya habari ili nyimbo zao zichezwe.
Hitmaker huyo wa “Yoola” amesema mastaa wengi nchini uganda hawana vipaji kwani wamekuwa wakizitangaza nyimbo ambazo hazina ubora kwa kuwalipa madejaay wa vituo vya redio na runinga.
Ikumbukwe pia Juzi kati wasanii kama Naira Ali na Sama Sojah aliwatolea uvivu baadhi ya wasanii wanaolipa vyombo vya habari ili kazi zao zichezwe