Staa wa muziki nchini Arrow Boy amefunguka ishu ya mpenzi wake nadia mukami kubadilisha dini kutoka ukristo kwenda uislamu.
Katika mahojiano yake hivi karibuni baada ya kuwasili kutoka nchini Ethiopia ambako alienda kwa ajili ya show yake, Arrow Boy amesema hana mpango kumfanya Nadia Mukami abadilishe dini hasa wakati wanaelekea kufunga ndoa yao kwa kuwa upendo ndio kitu kilichowaleta pamoja.
Mbali na hayo Arrow Boy kwa mara ya kwanza amekiri hadharani kutokuwa mwanachama wa chama cha muziki na hakimiliki nchini MCK huku akitoa changamoto kwa wasanii wa kenya kuacha kuifanya bodi ya PRISK mzaha mtandaoni na badala yake waungane kwa ajili ya kuleta mabadilliko kwenye bodi zilizopewa jukumu za kusimamia mirabaha ya wasanii.
Utakumbuka Arrow boy ambaye vizuri na album yake ya Focus kwa sasa anajianda kuanza tour yake ya muziki barani ulaya hivi karibuni.