You are currently viewing ARROW BOY AKANUSHA MADAI YA KUTUMIA KIKI KUTANGAZA MUZIKI WAKE

ARROW BOY AKANUSHA MADAI YA KUTUMIA KIKI KUTANGAZA MUZIKI WAKE

Msanii nyota nchini Arrow Boy, amesema yeye haitaji kiki ili kazi zake ziweze kufanya vizuri sokoni, tofauti na wasanii wengi wa sasa hivi.

Akiwa Instagram Live Arrow Boy amesema kazi nzuri inajitangaza yenyewe bila kiki, kwani msanii anaweza tengeneza kiki kubwa alafu kazi yake ikawa haina ubora, na kushusha hadhi ya muziki wake.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Unconditional Love” amesema kuwa wasanii wengi wamejikita kwenye kutafuta kiki badala ya kuwapa mashabiki ladha tofauti na kusisitiza kwamba dhana ya kiki inapaswa kufutika ili kila mtu afanye kazi nzuri.

Hata hivyo amewataka wasanii wenzake waache kutafuta ‘kiki’ ili kupata majina makubwa kwenye muziki bali wajikite kwenye kutengeza kazi nzuri.

Kauli ya Arrow Boy imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kutilia ziara yake ya “Meet The People Tour” kwenye baadhi ya mitaa jijini Nairobi ambapo alipata fursa ya kula chakula na kupiga stori mashabiki zake lakini pia aliwalipia nauli, kitu ambacho kiliwafanya walimwengu kuhoji kuwa alikuwa anatumia jambo hilo kutafuta kiki kwa ajili ya kuitangaza album yake mpya iitwayo Focus itakayoingia sokoni Machi 12 mwaka wa 2022.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke