You are currently viewing ARROW BOY AMVUA NGUO JALANG’O, AMTAKA AACHE KUFUATILIA MAISHA YAKE NA NADIA MUKAMI

ARROW BOY AMVUA NGUO JALANG’O, AMTAKA AACHE KUFUATILIA MAISHA YAKE NA NADIA MUKAMI

Staa wa muziki nchini Arrow Boy kwa mara nyingine amekanusha tetesi za mchumba wake Nadia Mukami kuwa na uja uzito wake.

Hii ni baada ya mchekeshaji Jalang’o kwenye kipindi cha Jalas and Kamene in the morning kinachoruka kupitia Kiss 100 kusisitiza kuwa Nadia Mukami ni mjamzito na alithibitisha hilo wakati wapenzi wawili hao walimtembelea kijiji kwao.

Jalango alienda mbali zaidi na kumshauri Nadia Mukami aache ishu ya kuficha uja uzito kwa umma kwani hivi karibuni itajulikana tu.

Sasa akijibu hilo Arrow Boy kupitia instastory ameandika ujumbe unaosomeka “2022 Wanaume Tupunguze Mshene Bana biashara Haikuhusu achana nayo Kabisa shugulika na maisha yako” ujumbe ambao umetafsiri kumlenga moja kwa moja Jalang’o.

Juzi kati Nadia Mukami aliripotiwa kuwa na uja uzito wa Arrow Boy hii ni baada ya kuonekana akitumbuiza kwenye show moja akiwa amevalia mavazi makubwa jambo ambalo liliwafanya wajuzi wa mambo kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa hitmaker huyo wa “Roho Mbaya” ni mjamzito.

Hata hivyo Nadia Mukami kupitia Instagram page yake amenyosha maelezo kwa kupost picha ambayo imezima kabisa tetesi za kuwa na uja uzito.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke