You are currently viewing ARROW BOY ATANGAZA RASMI MAHALA PATAKAPO FANYIKA UZINDUZI WA ALBUM YAKE MPYA

ARROW BOY ATANGAZA RASMI MAHALA PATAKAPO FANYIKA UZINDUZI WA ALBUM YAKE MPYA

Staa wa muziki nchini Arrow Boy ametangaza rasmi mahala patakapo fanyika uzinduzi wa Album yake mpya iitwayo ‘Focus’.

Kupitia ukurasa wake wa instagram mkali huyo wa ngoma ya Unconditional ametujuza kuwa Album hiyo ambayo itaachiwa rasmi tarehe 12 mwezi huu, uzinduzi wake utafanyika Katika ukumbi wa ‘The Junction Mall’ uliopo , Jijini Nairobi.

Bosi huyo wa lebo ya muziki ya Utembe World amewataka mashibiki ku-pre-order tiketi za kuhudhuri uzinduzi wa album yake ya Focus kupitia wavuti mtickects.com huku akiwataja  Nadia Mukami, Sanaipei Tande, Iyaani, Kristoff, Hart The Band, na Dufla Diligon kama baadhi ya wasanii watakaomsindikiza kwenye uzinduzi wa album yake hiyo.

Licha ya kuweka wazi jina na cover ya album yake mpya, Arrow Boy hajatuambia idadi ya ngoma na wasanii aliowashirikisha kwenye album yake ya Focus.

Focus album inaenda kuwa album ya pili kwa mtu mzima Arrow Boy baada ya Hatua iliyotoka mwaka wa 2019.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke