You are currently viewing ARROW BOY AWAPA SOMO VIJANA WA KIUME KUHUSU MPANGO WA UZAZI

ARROW BOY AWAPA SOMO VIJANA WA KIUME KUHUSU MPANGO WA UZAZI

Hitmaker wa “Enjoy”, Msanii Arrow Boy ametoa changamoto kwa vijana wa kiume kujipanga kimawazo na kifedha kabla ya kuwapa wapenzi wao uja uzito.

Kupitia kurasa zake za mitadao ya kijamii, Arrow Boy amesema safari ya uja uzito inakuja na changamoto nyingi, hivyo ni vyema kwa kijana wa kiume kutumia kinga kama hayuko tayari kubeba mzigo wa uzazi.

Bosi huyo wa Utembe World ameenda mbali Zaidi na kuhoji kuwa ikitokea kijana wa kiume amempa binti wa watu uja uzito bila kutarajia anapaswa kutoa ushirikiano kwenye suala la kutoa matunzo kwa mama pamoja na mtoto.

“Boychild kama hauko ready na hizi mbwe mbwe za pregnancy journey tumia tu jwala na ukijipata hapa please cooperate #Kaiwangu trending on YouTube”. Ameandika Arrow Boy.

Utakumbuka kipindi Nadia Mukami alikuwa mja mzito, Arrow boy alikiri hadharani kupitia changamoto kibao kwenye safari yake ya uja uzito lakini mwisho wa siku alifanikiwa kumliwaza baby mama wake huyo kwa kumpa mahitaji ya msingi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke