You are currently viewing ASAP ROCKY AACHIWA UHURU KWA DHAMANA

ASAP ROCKY AACHIWA UHURU KWA DHAMANA

Rapa kutoka marekani A$AP Rocky amefanikiwa kuachiwa kwa dhamana ya shilling million 55 za Kenya.

Kwa mujibu wa TMZ Mpenzi wake Rihanna ndiye aliyempigania hadi akatoka polisi kwa kulipa kiasi hicho cha pesa.

A$AP Rocky alikamatwa Aprili 20 wakati akiwasili katika uwanja wa ndege wa Los Angeles akitokea visiwani Barbados na ndege binafsi akiwa pamoja na mpenzi wake Rihanna.

Ikumbukwe Rocky alitiwa mbaroni na Polisi kufuatia tukio la Novemba mwaka jana ambalo lilihusisha silaha ambapo mtu mmoja alidai rapa huyo alimpiga risasi takriban 4 kwenye mkono wake wa kushoto na kumsababishia majeraha.

Hata hivyo polisi walipata kibali cha kupekua nyumba ya A$AP Rocky baada ya mlalamikaji kutoa ushahidi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke