Rapa kutoka Marekani Asap Rocky amemchana Chris Brown kwenye wimbo wake mpya (D.M.B) ambao umetoka Mei 5 Mwaka huu.
Kwenye moja ya verse katika ngoma hiyo, A$AP Rocky amesema “I don’t beat my b*tch, I need my b*tch.” akihusisha na tukio la Chris Brown kumpiga Rihanna mwaka 2009.
Jina la wimbo huo limefupishwa kuwa (D.M.B) ikiwa na maana ya “DAT$ MAH B!*$H.”
Utakumbuka mwaka 2009 Chris Brown alimpiga Rihanna wakiwa kwenye gari na kumsababishia michubuko usoni kiasi cha kupelekea wawili hao kuachana.
Chris Brown alihukumiwa kifungo cha nje miaka 5 huku akiwa chini ya uangalizi pamoja na kufanya kazi za Kijamii.