You are currently viewing ASAP ROCKY ATUPWA JELA KWA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA

ASAP ROCKY ATUPWA JELA KWA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA

Rapa kutoka Marekani Asap Rocky ametiwa mbaroni na polisi wakati akiwasili katika uwanja wa ndege wa Los Angeles Aprili 20 akitokea visiwani Barbados na ndege binafsi.

Kwa mujibu wa mashahidi waliotazama tukio hilo, wameiambia tovuti ya TMZ kwamba rapa huyo alitiwa pingu na kuondoka pamoja na polisi.

NBC wameripoti kwamba, Asap Rocky amekamatwa kufuatia tukio la November mwaka 2021 ambalo lilihusisha silaha ambapo mtu mmoja alidai rapa huyo alimpiga risasi 4 kwenye mkono wake wa kushoto.

Haijafahamika bado tukio hilo lilitokea wapi lakini inasemekana kuwa kuna watu wamefungua kesi ya kushambuliwa na Rapa huyo mwaka wa 2021.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke