Mwanamuziki kutoka Marekani Ashanti ametoboa siri ambayo wengi walikuwa hawaifahamu, amekiri kuwahi kupitia changamoto kwenye muziki wake ikiwemo ya kuombwa rushwa ya ngono na Mtayarishaji wa Muziki ili tu apate nafasi ya kurekodi wimbo.
Kwenye mahojiano na The Breakfast Club, Ashanti amekaririwa akisema, baada ya kurekodi nyimbo mbili na Mtayarishaji huyo, ilifika wakati wa kutaka kuziweka kwenye Album na hapo ndipo Jamaa alimwambia anamtaka kimapenzi na kama akikataa ombi hilo, basi atalipia ($40k) zaidi ya KSh. Milioni 4.9 kwa kila wimbo.