You are currently viewing AVRIL AFUNGUKA JUU YA UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

AVRIL AFUNGUKA JUU YA UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

Staa wa muziki nchini Avril amewajibu wanaodai kuwa hajakuwa akiachia nyimbo kila mara licha ya kuwa na kipaji kikubwa cha muziki.

Katika mahojiano na Mungai Eve, Avril amesema kuwa amekuwa akiachia nyimbo kila mwaka ila watu hawajakuwa wakifuatilia kazi zake kama kipindi cha nyuma kwa sababu hapendi suala la kutengeneza matukio kwa ajili ya kuzungumziwa mtandaoni.

Aidha amefunguka ya wimbo wake mpya kutopata wafuasi wengi kwenye mtandao wa youtube kwa kusema kwamba alijihisi vibaya wakati watu walianza kumfanyia mzaha mtandaoni huku akidai kuwa ni changamoto ya kazi.

Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa m amedokeza ujio wa ep mpya ya pamoja na prodyuza Saint P ambayo kwa mujibu wake itaingia sokoni hivi karibuni.

Avril ambaye yupo chini ya lebo ya muziki ya Digit One Music anafanya vizuri na album yake ya Spirit ambayo ina zaidi ya streams millioni 2 kwenye mtandao wa Boomplay.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke