Mwanamuziki Avril amefunguka madai ya kuitosa kolabo ya msanii mwenzake Mr. Seed mwaka wa 2021.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Avril amesema hakuweza kufanya kazi ya pamoja na msanii huyo kwa sababu kipindi hicho alikuwa ameshikika na masuala ya kuitayarisha album yake ya Spirit.
Hitmaker huyo wa “Chokoza” ameahidi kufanikisha kolabo yake na Mr. Seed hivi karibuni pindi tu ratiba zao zitakapokuwa sawa.
Kauli yake imekuja mara baada ya mr. Seed kudai kuwa Avril amekuwa akikwepa kufanya nae kazi kwa muda wa miaka minne sasa licha ya kumkumbusha kila mara.
Haikushia hapo alienda mbali zaidi na kudai kuwa wimbo wake wa ndoa alipaswa kumshirikisha Avril lakini kilichotokea na kumvunja moyo ni kitendo cha msanii huyo kuanza kumchunia kwa kutojibu meseji zake, hivyo akaamua kurekodi wimbo huo na mwigizaji Kate the Actress.