You are currently viewing AY MASTA APATA TUZO YOUTUBE

AY MASTA APATA TUZO YOUTUBE

Msanii mkongwe kwenye muziki wa Bongofleva AY ametunukiwa tuzo ya Silver Plaque na mtandao wa Youtube baada ya kufikisha jumla ya subscribers laki moja kwenye channel yake.

AY ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia kazi zake za muziki huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi.

“Finally i got my @youtube Plaque…Round hii hailali ni Kazi juu ya Kazi,Content Juu ya Content tufike wanafamilia 500,000 mpaka 1,000,000 na kuendelea..Kazi mpya soon so fanya Ku SUBSCRIBE My Channel AY MASTA uwe wa kwanza kuona kazi zangu zijazo.ONE”, Ameandika Instagram.

Channel ya youtube ya AY ilifunguliwa rasmi Oktoba 26 mwaka wa 2011 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 20.8 huku ikiwa na jumla ya subscribers 113, 000.

Itakumbukwa tuzo ya Silver Plaque huwa inatolewa kwa wanamuziki au watu maarufu kwenye mtandao wa Youtube ambao hujizolea zaidi ya subcribers laki moja.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke