You are currently viewing Azam yathibitisha kumsajili Fei Toto

Azam yathibitisha kumsajili Fei Toto

Kaimu Afisa Habari wa Azam FC, Hashim Ibwe amethibitisha kuwa matajiri hao wa Dar es Salaam wamefanikiwa kunasa saini ya kiungo machachari wa mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC, Feisal Salum baada kuvunja mkataba na mabingwa hao.

Kwa mujibu wa Ibwe, kila kitu kipo sawa na mchezaji huyo ni wao kwa sasa huku wakisubiri muda wa kumtangaza kwa mashabiki na wapenda soka

“Kila kitu cheupe na tunasubiri tu utaratibu wa kumtangaza Fei kama mchezaji wetu hulali,” ameongeza Ibwe.

Katika taarifa ambazo hazijathibitishwa, Fei Toto ameripotiwa kuilipa Yanga kitita cha shilingi milioni 112 ili kung’oka Jangwani ikiwa ni shilingi milioni 100 kama pesa za usajili na shilingi milioni 12 kama mshahara wa miezi mitatu ijayo.

Wakati hayo yakijiri, Yanga na Azam zitashuka dimbani Desemba 25, 2022 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao utaanza saa 8:15PM usiku.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke