You are currently viewing AZEALIA BANKS AMCHANA JAY Z KISA MEGAN THEE STALLION KUMTOSA RAFIKI YAKE CARA DELEVINGNE

AZEALIA BANKS AMCHANA JAY Z KISA MEGAN THEE STALLION KUMTOSA RAFIKI YAKE CARA DELEVINGNE

Mwanamuziki kutoka Marekani Azealia Banks ameamua kumvua nguo msanii mwenzake Megan Thee Stallion.

Kupitia mfululizo wa posts zake kwenye mtandao wa Twitter hitmaker huyo wa ngoma ya “212” ametoa ya moyoni kwa kusema kwamba tukio la Megan Thee Stallion kudai kuwa amepigwa risasi na Tory Lanez, ni mpango wa kimasoko ambao umefanywa na Jay-Z.

Azealia ameamua kumuingiza Jay-Z kwenye sakata hilo kutokana na kumsimamia Megan Thee Stallion chini ya Roc Nation.

Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema mikakati ya Jay-Z kuwauza wasanii wa Kike siku zote huwa anatengeneza mikasa waseme wamenyanyaswa na wapenzi wao, pia huwatumia kama ajenda kwenye jambo lolote.

Kauli ya Azealia Banks imekuja mara baada ya Megan Thee Stallion kuondoa picha ya rafiki yake wa karibu Cara Delevingne katika picha ya pamoja waliyopiga na Doja Cat kwenye hafla ya tuzo za Billboard 2022.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke