Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Aziz Azion, ametangaza kwamba ana mpango wa kuja na tamasha la muziki la One Decade Concert kuadhimisha miaka 10 ya uwepo wake kwenye muziki baada ya katazo la kufanya matamasha ya muziki litakapoondolewa nchini uganda.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amedokeza kuwa kiingilio cha tamasha hilo litakuwa shillingi laki tano za kenya katika sehemu ambayo ataweka wazi hivi karibuni baada kukamilisha taratibu za kuandaa tamasha hilo.
Hitmaker huyo wa My Oxygen amesema alipaswa kufanya tamasha hilo mwaka wa 2019 lakini kwa sababu ya maswala kadhaa ambayo yalikuywa nje ya uwezo wake, alilazimika kuahirisha hadi mwaka wa 2020.
Mwaka wa 2020 bado, tamasha hilo lilifeli kufanyika kufuatia kuzuka kwa janga la Corona ambayo ililemaza shughuli zote za kibiashara ulimwenguni kote.