You are currently viewing B CLASSIC AACHIA KAZI YAKE YA MWISHO

B CLASSIC AACHIA KAZI YAKE YA MWISHO

Msanii wa muziki nchini Kenya, Dennis Manja maarufu kama B Classic ameachia wimbo wake wa mwisho baada ya kutangaza nia yake ya kutaka kuacha muziki.
 
B Classic alidai kuwa anaacha muziki na kugeukia kazi ya ufundi wa magari baada ya kutoridhishwa na mapokezi ya kazi zake pindi anapoachia muziki mpya.
 
B Classic mkali wa wimbo wa Pisi Kali uliofanya vizuri mapema mwezi Agosti mwaka huu, ameachia  ‘Utawezana Kweli’, wimbo anaodai kuwa itakuwa kazi yake ya mwisho.
 
Wimbo huo umetayarishwa na Prodyuza Denzel huku video ikaongozwa na Director Rahim chini ya lebo ya muziki ya Champions Studio yenye makao yake jijini Nairobi.
 
 
 
 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke