You are currently viewing B2C ENT WAAHIRISHA ZIARA YAO YA MUZIKI BARANI ULAYA

B2C ENT WAAHIRISHA ZIARA YAO YA MUZIKI BARANI ULAYA

Wasanii wa Kundi la B2C Entertainment kutoka Uganda wametangaza kusitisha ziara yao ya muziki iliyopaswa kuanza rasmi mwezi huu wa Juni huko barani Ulaya.

Kupitia taarifa waliyochapisha kwenye mitandao yao ya kijamii wasanii wa kundi hilo kwa masikitiko makubwa wamesema wamelazimika kupiga chini show hiyo kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao.

Hata hivyo wamewaomba radhi mashabiki wao wote ambao kwa njia moja au nyingine wameathirika na uamuzi wao huo huku wakiahidi kufanya ziara nyingine kama hiyo barani Ulaya siku za mbeleni.

Utakumbuka B2C walipaswa kufanya shows zao nchini Uturuki, Ujerumani na Uingereza Juni 4, 5 na 6 mtawalia.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke