Wasanii wa Kundi la muziki la B2C wamefunguka sababu za kutofanya maonesho yao ya muziki nje ya nchi ya uganda.
Katika mahojiano yao hivi karibuni wasanii wa B2C ambalo linaundwa na wasanii watatu wamesema mmoja wao hana pasipoti hivyo imekuwa changamoto kwao kusafiri nje ya nchi ikizingatiwa kuwa hawezi kutumbuiza au kufanya onesho lolote la muziki bila mmoja wao.
Kauli yao imekuja mara baada ya kusitisha show yao waliopaswa kuifanya nchini Uingereza mapema mwezi Juni kutokana na changamoto ya kupata hati ya usafiri.
Kwa sasa wapo kwenye matayarisho ya onesho lao la muziki litakalofanyika Agosti 19 mwaka huu huko Freedom City viungani mwa jiji la Kampala.